Wednesday 2 October 2013

UKISTAAJABU YA MUSA..............

UKISTAAJABU YA MUSA...............


  • NI NYANI JAMII YA NGEDERE AISHIE KATIKA FAMILIA MOJA NA BINADAMU
  • NI WATANZANIA WACHACHE WENYE "HOBBY" NA UPENDO KWA WANYAMA
  • HUENDA SALUNI,HULA PAMOJA NA BINADAMU NA PIA HUPATIWA MATIBABU KAMA BINADAMU.
  • ANAITWA JACKSON "JACKY" 
 JL Company ilivutiwa na maisha ya Jacky na imedhamiria kumsaidia katika chakula na dawa ila pia mashuka ya kulalia na godoro. 

Endelea Kusoma na Ushuhudie Maajabu ya Jacky katika.................


Happy ndie mlezi mkuu wa Jacky. wakiwa njiani kuelekea saluni pamoja kwa. Jacky ana umri wa mwaka mmoja sasa. 
Jacky akiandaliwa kwa ajili ya kuogeshwa. Ngedere huyu anatabia kama mtoto mdogo, huchagua mtu anaemfahamu amuogeshe na huwa mkali sana na hata kugoma kuoga endapo ataogeshwa na mtu asiemfahamu. ni mcheshi sana na hupenda kucheza na kila mtu.
Jacky baada ya kuoga akiwa na mlezi wake.
Kadanganyishiwa mkate ili apakwe mafuta na kuchanwa nywele (manyoya.)
Mtoto akilia mama hulazimika kumnyonyesha au kumpa uji. Jacky pia alilia njaa wakiwa wanaendelea na shughuli za saluni hivyo alipewa chakula kama aonekanavyo katika picha.ameketi kwa nidhamu na utulivu akila   ( table manners applied)
Jacky ni rafiki wa watoto na mara nyingine si kucheza pamoja tu bali hula pamoja.


"Jacky ni sehemu ya familia yangu, tunakula pamoja na kucheza pamoja. Ni msafi sana kila asubuhi anapiga mswaki na anajua wapi ajisaidie haja ndogo na kubwa. Itokeapo kaumwa ni rahisi kumgundua kwani huwa mtulivu na hupunguza kula au hugoma kabisa kula. Na ameshawahi umia pia, alipigwa na gongo na mtoto wa jirani kitu kilichopelekea kuvuja damu nyingi puani na kuvimba mguu. Nilimchua mguu na kumpa dawa ya maumivu ( diclofenac) lakini alimchukia sana yule mtoto na hata alipojaribu siku nyingine kucheza nae Jacky alimng'ata kwa kujihami." alisema Happy.
Haya ni maajabu kwa watanzania wengi. Je, wewe ungeweza?

No comments: