- Uanachama wa Zitto Changamoto Nzito.
- Kweli siasa mchezo mchafu.........
UANACHAMA
wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe umetajwa kuwa
‘kaa la moto’ kwa uongozi wa chama hicho hata kabla ya kiongozi huyo
kujibu mashitaka 11 yanayomkabili ili kunusuru uanachama wake.
Mh. Zitto Kabwe. |
Duru
za siasa ndani ya chama hicho, zinasema Chadema haiko tayari
kukabiliana na mtikisiko wa Zitto kuvuliwa uanachama, kwa kuwa hatua ya
kuvuliwa madaraka tayari imegharimu umoja na utulivu wa chama hicho.
Taarifa
hizo zinasema kwa sasa kuanzia Kamati Kuu mpaka wanachama, kuna mpasuko
mkubwa ambao namna pekee ya kuuziba ni kumshawishi Zitto na Mwenyekiti
Freeman Mbowe, kupatana.
Hata
hivyo, wakati jitihada za kuwapatanisha zikiendelea, duru za siasa
zinaeleza kuwa kambi ya Mbowe ina wajumbe wanaoshinikiza kumtosa Zitto
na kuwa tayari kukabiliana na gharama zake.
Majimbo
Mtoa
habari wetu kutoka ndani ya Chadema anaeleza kuwa hofu kubwa iliyopo
kama Zitto atanyang’anywa uanachama, ni ukweli kuwa katika Uchaguzi Mkuu
wa 2015, wanaweza kupoteza majimbo mengi na kuipa mwanya CCM kupita
kirahisi.
“Ni
kweli huu si mgogoro wa kwanza kwa Chadema na mara zote viongozi
walipovuliwa madaraka kulitokea mtikisiko, lakini si kama huu wa Zitto…
mbaya zaidi, majimbo ya viongozi tuliowavua madaraka leo hii yamepokwa
na CCM, hatuko tayari kupoteza zaidi,” alisema mtoa habari huyo ambaye
hakuwa tayari kutajwa jina.
Akitoa
mfano, alisema mgogoro kati ya Chadema na Katibu Mkuu wa zamani Dk Aman
Kabourou, ndio ulisababisha jimbo la Kigoma Mjini lililokuwa moja ya
majimbo ya Chadema, leo hii kukaliwa na CCM.
Mbali
na Kigoma Mjini, mtoa habari huyo alikumbushia pia jimbo la Tarime,
alikokuwa Makamu Mwenyekiti, Chacha Wangwe, ambalo mbali na kushinda
katika uchaguzi mdogo baada ya kifo chake, leo linashikiliwa na CCM.
“Unajua
hata kwa Zitto (Kigoma Kaskazini) ukiangalia kama kweli tukimtosa, sina
hakika kama tutarejesha lile jimbo. Na hata kwa Arfi (Said, Makamu
Mwenyekiti aliyejiuzulu, Mbunge wa Mpanda Kati), kama yule mzee
tukimchezea hatuna chetu,” alisema.
Alipoulizwa
afafanue kuhusu mpasuko huo, alikataa na kuhoji: “Kwani wewe huoni,
mbona wenzenu wameandika mpasuko uliotokea katika Kamati Kuu?”
Mbali
na mtoa habari huyo, hata katika waraka unaodaiwa kusababisha mtafaruku
huo ambao Dk Kitilla Mkumbo alikiri kuuandaa, Chadema imetajwa kuwa na
udhaifu wa kushinda majimbo katika uchaguzi mdogo.
“Tangu
uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika uchaguzi mdogo mara nane,
lakini tumeshinda mara mbili tu sawa na asilimia 25,” alisema Dk Mkumbo
katika waraka wake.
Usuluhishi
Pamoja
na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kutangaza kumwandikia Zitto
mashitaka yake na kumpa siku 14 za kujibu, tayari kumeripotiwa kuwa
nyuma ya pazia chama hicho kimeamua kumwangukia Zitto yaishe, ikiwa ni
pamoja na kumwahidi cheo kikubwa kuliko Naibu Katibu Mkuu.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo katika uchaguzi mkuu wa Chadema Juni mwakani,
Zitto atashawishiwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti bila mpinzani
au na mpinzani dhaifu na Mbowe ataachiwa kugombea uenyekiti bila
mpinzani au na mpinzani dhaifu, lengo likiwa kurejesha umoja wakati
wakijiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015.Pia inadaiwa Zitto ataahidiwa kupewa fursa ya kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Wasira
Akizungumzia
mgogoro huo akiwa mkoani Kagera, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen
Wasira, alisema anajivuna kwamba ndani ya chama chake hakuna ubaguzi
kama ilivyo katika vyama vingine vya upinzani ambavyo alidai kiongozi wa juu lazima atoke kabila fulani.
Mh. Stephen Wasira. |
Alidai
katika baadhi ya vyama, ikitokea mtu ametoka kabila tofauti akataka
kugombea uongozi ngazi ya juu, kunazuka vurugu na kufukuzana kwa
visingizio vya kuvunja katiba za vyama hivyo.
“Mara
nyingi huwa natumia kauli ya Mwalimu Julius Nyerere kuwa ubaguzi ni
sawa na kula nyama ya mtu, ukiishaionja huiachi kwa hiyo wameionja
inawatafuna. “CCM hatuna sababu ya kushangilia matatizo yao na
hatuwaogopi wala hatutaki upinzani ufe, kwa sababu upinzani ni mfumo
ulio ndani ya nchi, ila nasi tuache makundi yanayotokana na uchaguzi,
ili tuendelee kushika Dola kama ilivyo ada yetu,” alisema Wasira.
Vyuo vikuu
Baadhi
ya wanachama wa Chadema, wakiwamo wanafunzi wa vyuo vikuu, walikutana
Dar es Salaam jana na kutangaza mgogoro wa kiutawala kati ya wapigania
demokrasia ndani ya chama hicho na wahafidhina.
Wanachama
hao waasi ambao walisema ni wapigania demokrasia ndani ya chama hicho;
lakini kwa tafsiri ya viongozi wa Chadema ni ‘wahaini’, wametangaza
kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wanachama wa chama hicho wakatae baadhi
ya watu waliopandikizwa kwa kukaimishwa nafasi za uenyekiti kwa manufaa
ya wahafidhina.
Baadhi
ya wanachama hao wakiongozwa na Greyson Nyakarungu, walidai wanatambua
kuwa mgogoro ndani ya Chadema umetokana na Mwenyekiti Mbowe kutamani
kuendelea kuongoza chama kwa gharama yoyote.
Nyakarungu
alidai Mbowe anatamani aendelee kutawala hivyo kuzunguka katika baadhi
ya mikoa na kuwaondoa katika nafasi zao viongozi waliochaguliwa
kidemokrasia, ambao wanaonekana kutomwunga mkono kwa kisingizio cha
kutowajibika.
Nyakarungu
ambaye alijiita Brigedia wa Uasi huo, alisema watu wote waliopenyezwa
kukaimu nafasi hizo za uongozi mikoani wajiondoe haraka “kabla
hatujawaondoa kwa nguvu.
“Sisi
tumeamua kama tulivyozunguka nchi nzima na kampeni ya Washa Taa Mchana,
tutazunguka nchi nzima kuwaambia wanachama ubovu huu wa wahafidhina.
“Tunamwonya Zitto na Dk Mkumbo tabia zao za kusema kuwa wanaheshimu
uamuzi wa CC huku wakijua ni nini kitatokea, waache mara moja, kwani
unyonge wa aina hii ni kuendelea kuruhusu baadhi ya watu kupora
rasilimali za chama,” alidai Nyakarungu.
Nyakarungu, Jeremia Fumbe wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Likapo Bakari ambaye alifukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma, walisema wao ni majeruhi wa kufinyangwa kwa demokrasia ndani ya chama hicho, na kila hoja ambayo wanatoa wamekuwa wanaitwa masalia ya Zitto.
Nyakarungu, Jeremia Fumbe wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Likapo Bakari ambaye alifukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma, walisema wao ni majeruhi wa kufinyangwa kwa demokrasia ndani ya chama hicho, na kila hoja ambayo wanatoa wamekuwa wanaitwa masalia ya Zitto.
Nyakarungu
alisema watu wote wanaoitwa wasaliti ndani ya chama hicho au wanaotumwa na CCM’ hoja yao imekuwa moja tu ya matumizi ya fedha za
chama hicho, hoja ambayo pia walidai imemgharimu Zitto.
“Tunafikia
hatua wahafidhina wanasema wazi kuwa ni bora chama kishuke daraja
kuliko kupewa mtu wa nje, mtu wa kuja, mtu wasiyemfahamu,” alisema
Nyakarungu na kusisitiza kuwa wanachama wa Chadema kutoka Mara na Kigoma
ndio wamekuwa wahanga zaidi.
Nyakarungu,
ambaye alidai alijiunga na chama hicho mwaka 2005 na kushiriki kujenga,
alisema kilichomponza Zitto ndani ya chama hicho ni kuhoji matumizi ya
chama hicho kupitia kamati ya Bunge ya PAC, ndio maana alishambuliwa
yeye binafsi wakati huo ulikuwa uamuzi wa Kamati ya Bunge.
“Viongozi
wetu wa Chadema wanahoji Serikali na matumizi ya fedha za walipa kodi
wakitaka uwazi na usawa, leo wanataka kutonywa mapema ili wafanye
marekebisho ya kuficha uovu wa matumizi ya pesa? “Zitto kama kiongozi
anayejipambanua asingeweza kuwatonya ili wafiche uchafu katika matumizi
ya fedha huku akitengeneza nafasi ya kuumiza vyama vingine, hii ni
dalili ya udikteta. Na kwa kuwa aligusa mkia wa mfalme nge ni lazima
ang’atwe,” alidai Nyakarungu.
Source: Habari Leo
No comments:
Post a Comment