Wednesday, 30 October 2013

INAGHARIMU KIASI GANI KUANZISHA BIASHARA?

  • wengi huchagua ujasiliamali?
  • Ni jinsi gani uanzishe biashara ndogo ndogo?

Video hii (Au Bofya Hapa uione kwenye Vimeo) inatueleza si tu mtu asie na kazi ndie awe mjasiliamali bali hata walioko maofisini wanajishughulisha. Utasikia ushauri pia kwa wanawake kutoka kwa Madam Shammy.


Watu wengi katika ulimwengu wa sasa,wawe waajiriwa ama lah! wamegundua ujasiliamali  ndio "BIG DEAL".Utajiuliza kwanini?

  1. Faida: Baina ya wajasiliamali waliopata na wanaoendelea kupata faida kubwa nchini Marekani ni pamoja na Bill Gate, mmiliki wa Microsoft Corporation na Sam Walton mmiliki na mwanzilishi wa Wal-malt. Unawezakuwa miongoni mwa watanzania wengi ambao pia hupata faida kubwa kila mwaka kwa shughuli za ujasiliamali.
  2. Fursa: Hii ni moja ya sababu kubwa inayohamasisha watu kuacha kazi na kujiajiri wenyewe. Fursa zipo ktk nyanja mbalimbali iwe kilimo, elimu, biashara, ujenzi n.k je, wewe ndoto yako ni kuwekeza au kuwa na biashara yako?acha kuota, amka!!
  3. Changamoto: Asilimia kubwa ya wajasiliamali hutafuta zaidi mafanikio kuliko uongozi au umaridadi. Ujasiliamali sio kamali, hasara ni moto na sehemu ya kukomaa (kukua) zaidi kama si kujifunza.
  4. Uhuru: Watu wengi hawanauhuru na furaha kufanya kazi katika kampuni au watu binafsi na hata serikalini kwa kuepuka presha na "stress" huanzisha na huridhika na shughuli zao binafsi.
  5. Ukosefu wa ajira: Vijana wengi wa kitanzania wameamka na hata kugeukia upande wa pili wa shilingi baada ya ukosefu wa ajira na kujikuta wakiendelea kuzunguka na bahasha zao bila mafanikio.
  6. Vipaji (Talent): Wapo walogundua kuwa kwa kuajiriwa wanakosa fursa ya kutumia vipaji vyao ambavyo vingiweza kuwalipa zaidi.
Fuatilia picha hizi zinazomhusu Kijana Zawadi na mwenzake walivyoweza kujiajiri hapa Jijini Mbeya 
                                                                                                                                    
Juu: Huyu ndiye Zawadi kijana alietokea kutembeza katika begi la mgongoni culture (cheni zilizotengenezwa kwa shanga na nyuzi, kofia) hadi kufungua ofisi yenye kutembelewa na idadi kubwa ya watalii, Arts and Tribues Tours.


Juu: seti ya kochi imetengenezwa kwa kamba za porini.


Juu: Stendi na vikapu vya maua vinavyotengenezwa kwa malighafi zipatikanazo hapa hapa nchini.



Kushoto: 'coffee table' inayotengenezwa pia kwa mianzi, miti na kamba za porini na kuuzwa kwa bei nafuu sana. 














Kulia: Ni vitambaa, posti kadi na picha zilizochorwa kwa mikono.



Kushoto: Viti vya asili vilivyochongwa kwa mninga.














  Jinsi ya kuanzisha biashara 

Biashara nyingi ndogo ndogo huanzia nyumbani lakini ili uwe na biashara yenye mafanikio zingatia yafuatayo;
  • Weka wazo la biashara unayotaka kufanya katika maandishi na mpangilio mzima wa jinsi unavyotaka biashara yako iwe.
  • Andaa mchanganuo wa biashara (business plan).
  • Uwe na mtaji haijalishi mkubwa au mdogo pamoja na rasilimali watu (employee or partners).
  • Tambua wateja wako, hali ya soko na sehemu soko lilipo.
  • Weka rekodi ya mahesabu ya shughuli zako (accounting). Hii itakusaidia kutambua kama unafanya biashara kwa kukua au hasara.  

No comments: