Saturday, 30 November 2013

MAAJABU: MAITI HUFUKULIWA NA KUBADILISHWA NGUO.

  • Ni huko kisiwani SULAWESI, Indonesia.
  • Zoezi hili hufanyika kila mwaka.
Image
KILA mwaka huko kaitika kisiwa cha Sulawesi, Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo na kuwatembeza kijini hapo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila ya ajabu inayoiitwa Ma’nene  ambayo wanaamini mtu akifa bado yuko nao kwa hiyo inawalizimu kufanya mambo hayo kama kuwabadilisha nguo.
Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.

Source: Michapo Blog.

No comments: