- Limeundwa kwa mawe.
- Ni imara na linamiaka mingi zaidi
- Halijawahi athiriwa na tetemeko la ardhi au mmomonyoko wa udongo
Daraja la Mungu liko Mbeya, Mbalizi katika kijiji cha Sisitila. Chakushangaza wenyeji wengi hawatambui kama ni kivutio kikubwa kwa wageni (watalii) kutokana na maajabu ya daraja hili.
Chini ya daraja hili kuna mto ambao umekua na manufaa makubwa kwa wakazi wa kijiji cha Sisitila na Wimba kwani wameweza kufanya kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga na vitalu vya miti pamoja kunyweshea mifugo. Kama inavyoonesha katika picha upande wa kulia ni mfereji ambao unatumika kuchukua maji kutoka katika mto na kupeleka shambani. Picha kushoto: Shamba la mbogamboga.
Kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya, kama mtakumbuka Disemba, 1997 wakati wa mvua kubwa za El Nino daraja la mto Mbalizi katika eneo la Mbalizi , Mbeya lilibomoka kwa mafuriko mbali ya kuwa na mifereji mitatu lakini DARAJA LA MUNGU halikutetereshwa na mvua wala mafuriko hayo............AJABU!!!!!
Yawezekana mizizi ya mti huu ni moja ya vizuizi vya mmomonyoko wa udongo katika daraja hilo.
Baadhi ya mifugo ikiswagwa kuelekea katika mto unaopita chini ya daraja la Mungu. |
Baadhi ya mawe yaliyochanganyika na udongo na kuunda daraja hilo. |
No comments:
Post a Comment